Pata taarifa kuu
ISRAEL-PALESTINA-USALAMA

Askari wa Israeli waongezwa kwenye mpaka na Ukanda wa Gaza

Serikali ya Israel imeongeza askari wake pembezoni mwa Ukanda wa Gaza ili kukabiliana na kuingia kwa raia wa Palestina nchini humo wakati wa maandamano makubwa katika ardhi ya palestina, ambayo yanaingia katika mwezi wa saba.

Hali ya machafuko yaendelea kushuhudiwa katika Ukanda wa Gaza, Palestina.
Hali ya machafuko yaendelea kushuhudiwa katika Ukanda wa Gaza, Palestina. REUTERS/Ibraheem Abu Mustafa/File photo
Matangazo ya kibiashara

Neno linalotumiwa na jeshi la Israeli ili kutangaza hatua hiyo kupitia taarifa yale haimaanishi operesheni kabambe ya kijeshi dhidi ya Ukanda wa Gaza, lakini inaonekana kuwa ni hatua muhimu pembezoni kwenye mpaka ili kuzuia jaribio lolote kutoka kwa Wapalestina kwa kuvuka uzio unaogawa nchi hiyo mbili wakati wa maandamano yao, ambayo yalianza mnamo mwezi Machi.

Tangu kuanza kwa maandamano hayo, angalau Wapalestina 193 wameuawa na vikosi vya usalama au vikosi vya ulinzi vya Israeli, kulingana na ripoti ya madaktari wa Gaza. Askari wa Israeli aliuawa kwa kipgwa risasi na raia wa Palestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.