Pata taarifa kuu
PALESTINA-MAREKANI-USHIRIKIANO

Mahmoud Abbas atoa maneno makali dhidi ya utawala wa Trump

Rais wa mamlaka ya Palestina, Mahamoud Abbas ameukashifu utawala wa rais Donald Trump, akitupilia mbali kuwa nchi hiyo ndio inaweza kuwa mpatanishi mkuu wa mizozo ya mashariki ya kati, kauli anayotoa siku mbili tu baada ya rais Trump kuahidi kupata suluhu kati ya Israel na Palestina.

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas wakati wa hotuba yake katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa Septemba 26, 2014.
Rais wa Palestina Mahmoud Abbas wakati wa hotuba yake katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa Septemba 26, 2014. REUTERS/Mike Segar
Matangazo ya kibiashara

Rais Abbas ametumia mkutano wa umoja wa Mataifa kuikashifu Marekani kwa uamuzi wake wa kufunga ofisi ya chama chake cha PLO jijini Washington na kuutambua mji wa Jerusalem kama makao makuu ya Israel.

Katika hotuba yake ambayo alitumia muda mwingi kuikashifu Marekani na Israel, rais Abbas amesisitiza kuwa mji wa Jerusalem hauuzwi! Kauli ambayo ilipokelwa kwa makofi ya wajumbe waliohudhuria kikao cha siku ya Alhamisi wiki hii.

Rais Abbas ameendelea kusisitiza nchi yake kutokubaliana na mapendekezo yoyote ya Marekani kuhusu upatanishi wake kwenye eneo la mashariki ya kati, kauli inayozidisha sintofahamu zaid kati yake na Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.