Pata taarifa kuu
SYRIA-SAUDI ARABIA-MAREKANI-USALAMA

Saudi Arabia yaahidi kutoa dola milioni 100 kwa kurejesha utulivu Syria

Marekani imekaribisha hatua ya Saudi Arabia ya kuchangia dola milioni 100 (sawa na euro milioni 87.8 ) ili kusaidia kuimarisha usalama katika maeneo ya Syria ambayo hayadhibitiwi na kundi la Islamic State (IS), wizara ya mambo ya nje ya Marekani imebaini.

Raqqa moja ya maeneo yaliyokua yakidhibitiwa na kundi la Islamic Sate (IS) Syria.
Raqqa moja ya maeneo yaliyokua yakidhibitiwa na kundi la Islamic Sate (IS) Syria. REUTERS/Rodi Said
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hili linakuja wakati ambapo utawala wa Donald Trump una mpango wa kupunguza fedha zinazowekwa katika mpango wa msaadakwa nchi za Mashariki ya Kati, ikiwa ni pamoja na Syria na Ukanda wa Gaza.

Huu ni "mchango mkubwa, muhimu kwa ajili ya utulivu na juhudi za kwanza za ujenzi," wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesem akatika taarifa kuhusu msaada uliotolewa na Saudi Arabia. "Msaada huu unakuja wakati muafaka wa kampeni."

Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, maeneo yanayodhibitiwa na kundi la Islamic State (IS) nchini Syria yametengwa kwa mita mraba 1,000 na watu karibu 150,000 waliweza kurudi katika mji wa Raqqa baada ya wapiganaji wa kundi hilo kuutoroka mji huo.

Washirika wa Marekani wanapaswa kuchangia kuimarisha utulivu na usalama katika kanda hiyo, wizara ya mambo ya nje ya Marekani imeongeza katika taarifa hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.