Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Mashariki ya Kati

Watoto 29 waangamia katika mashambulizi ya anga Yemen

media Watoto waliojeruhiwa katika shambulio la nga la ndege za muungano wa nchi unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya waasi wa Kihouthi, Alhamisi, Agosti 9, 2018. REUTERS/Naif Rahma

Umoja wa Mataifa untaka uchunguzi binafsi na wa haraka kufanyika baada ya kutokea kwa shambulizi la bomu Kaskazini mwa Yemen na kuwauwa watoto 29.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress ametoa wito huo, huku akitoa wito kwa pande zote zinazohusika katika vita nchini humo kuheshimu sheria za Kimataifa.

Aidha, Guteress asema ni muhimu sana kwa wanaopigana kuhakikisha kuwa hawawalengi raia wa kawaida na kutozuia misaada ya kibinadamu kuwafikia.

Wito huu umekuja wakati huu muungano wa nchi zinazoongozwa na Saudi Arabia kushukiwa kuwa nyuma ya shambilizi hilo baya katika siku za hivi karibuni.

Walioshuhudia shambulizi hilo wanasema wanajeshi hao wakiongozwa na Saudi Arabia walilenga basi lilolokuwa na wanafunzi katika eneo hilo ambalo lina waasi wa Kihouthi.

Shirika la Kimataifa la msalaba mwekundi limesema watoto wote waliopoteza maisha, walikuwa chini ya miaka 15.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana