Pata taarifa kuu
SAUDI ARABIA-CANADA-USHIRIKIANO-HAKI

Saudi Arabia yamfukuza balozi wa Canada

Serikali ya Saudi Arabia imechukua hatua ya kumfukuza balozi wa Canada baada ya kumpa saa 24 kuondoka nchini humo, huku ikimuita balozi wake huko Ottawa. Mahusiano ya kibiashara na Canada pia yamesimamishwa. Serikali ya Canada haijajibu.

Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau akiambatana na Waziri wake wa Mambo ya Nje Chrystia Freeland Mei 31, 2018.
Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau akiambatana na Waziri wake wa Mambo ya Nje Chrystia Freeland Mei 31, 2018. REUTERS/Chris Wattie
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja siku chache baada ya serikali ya Canada kukosoa hatua ya Saudi Arabia ya kuwakamata wanaharakati kadhaa wanaotetea haki za wanawake.

Rasmi, serikali ya Canada haijajibu.

Saudi Arabia haikufurahishwa na tangazo la Canada, siku ya Ijumaa, la kutaka wanaharakati wa wa haki za wanawake kuachiliwa huru mara moja.

Siku ya Alhamisi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada Chrystia Freeland, katika ukurasa wake wa Twitter aliandika kuwa ana wasiwasi kuhusu kufungwa kwa wanawake hawa, hasa Samar Badawi.

Bi Badawi amekuwa akitoa wito wa kumalizika mfumo wa wanaume kuwasindikiza wanawake kila wanapokwenda.

Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ilisema haiwezi kamwe kukubali kuingiliwa kwa masuala ya ndani ya nchi yao.

Mwanaharakati huyu anayetetea usawa wa kijinsia ni dada wa mwanablogu Raif Badawi, ambaye amefungwa nchini Saudi Arabia kwa miaka sita kwa kosa la kukosoa Uislam. Mke wake na watoto zake watatu wanaishi mjini Quebec, nchini Canada.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.