Pata taarifa kuu
YEMEN-UN-USALAMA

Mazungumzo ya amani ya Yemen kuanza Geneva Septemba 6

Awamu ya kwanza ya mazungumzo baina ya pande kinzani itafanyika tarehe 6 mwezi ujao  mjini Geneva, Uswisi. Mjumbe maalum wa Katibu  Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Yemen, Martin  Griffiths ametangaza tarehe hiyo. 

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu kwa Yemen, Martin Griffiths.
Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu kwa Yemen, Martin Griffiths. REUTERS/Khaled Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Bw Griffiths ametangaza tarehe hiyo akiwasilisha mapendekezo yake mbalimbali kusuhu jinsi ya kumaliza mzozo wa Yemen uliodumu kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.

Amesema amefikia hatua hiyo baada ya mashauriano na pande zote husika nchini Yemen, ikiwemo pande kinzani, mashirika ya kiraia na kwamba bado anaendelea na mashauriano na pande nyinginezo.

Kwa mantiki hiyo ameomba wajumbe wa Baraza la Usalama kuunga mkono jitihada zake za kufanikisha mazungumzo hayo yatakayofanyika mjini Geneva.

Wajumbe wametakiwa kutasaidia kufanikisha kusitisha mapigano yanayoendelea kwenye bandari ya Hudaidah na kuepusha bahari ya Sham dhidi ya mgogoro huo wa Yemen.

Bw Griffiths pia ametaka kuungwa mkono kwa hatua ambazo zinarejesha matumaini kwa wananchi wa Yemen.

Akizungumzia hali halisi nchini Yemen hivi sasa hususan matumizi ya bandari ya Hudaidah ambayo Umoja wa Mataifa iliafikiana na Ansar Allah kiongozi wa wapiganaji wa kihouthi , Bwana Griffiths amesema bado kuna mkwamo kwenye kufanikisha makubaliano kati yao.

Mkutano kuhusu mchatako  wa amani wa Yemen ulianzishwa  miaka 2 iliyopita chini ya uongozi wa mfalme Sheikh Jaber al-Ahmad al-Sabah wa Kuwait ambaye alijenga msingi wa mazungumzo yanayoendela hivi sasa .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.