Pata taarifa kuu
PAKISTANI-UCHAGUZI-USALAMA

Ishirini wauawa katika mlipuko nchini Pakistan

Watu ishirini wameuawa katika mlipuko uliotokea Jumatano wiki hii katika mji wa Quetta kusini magharibi mwa Pakistan, shambulio ambalo limekua limelenga gari la polisi, amesema msemaji wa hospitali katika mji huo. Shambulio hilo linatokea wakati ambapo kunafanyika uchaguzi wa wabunge nchini humo.

Watu ishirini waangamia katika mlipuko siku ya uchaguzi huko Quetta, Pakistan.
Watu ishirini waangamia katika mlipuko siku ya uchaguzi huko Quetta, Pakistan. REUTERS/Naseer Ahmed
Matangazo ya kibiashara

"Miili karibu 20 na watu 28 waliojeruhiwa wamepelekwa hospitali," amesema Daktari Wassim Baïg.

Mlipuko ulitokea karibu na kituo cha kupigia kura, shahidi mmoja ameliambia shirika la habari la Reuters huko Quetta, mji mkuu wa jimbo la Baluchistan.

Kwa mujibu wa Geo TV, moja ya televisheni nchini humo, idadi ya watu waliopoteza maisha ni 22 wakati ambapo televisheni ya Samaa TV imearifu kwamba watu 20 wameuawa katika mlipuko huo, na kuongeza kwamba mshambuliaji wa kujitoa mhanga ndio alitekeleza shambulio hilo.

Shambulio hilo linatokea wakati wananchi wa Pakistani wanapiga kura leo Jumatano katika uchaguzi wa wabunge unaodaiwa kuwa mkali kati ya chama cha Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI) kinachoongozwa na aliyekuwa bingwa wa kriketi Imran Khan na chama cha Pakistan Muslim League-Nawaz (PML-N) cha Waziri Mkuu wa zamani Nawaz Sharif.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.