Pata taarifa kuu
UTURUKI-ISRAELI-USHIRIKIANO

Erdogan: Israeli ni taifa la kifashisti na lenye ubaguzi duniani

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameitaja Israel kuwa ni taifa "la kiimla na lenye ubaguzi duniani" baada ya bunge la nchi hiyo kupiga kura wiki iliyopita kupitisha sheria inayoeleza nchi hiyo kama "taifa la Wayahudi" .

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan REUTERS/Umit Bektas
Matangazo ya kibiashara

"Hatua hii inaonyesha bila shaka kuwa Israel ni taifa la Kizayuni, taifa la kifashisti na lenye ubaguzi wa rangi duniani," amesema Erdogan katika hotuba yake mbele ya kundi lake la wabunge huko Ankara wakati ambapo wabunge wamepiga kelele wakisema "ilaaniwe Israeli".

Muswada wa sheria iliyopitishwa siku ya Alhamisi wiki iliyopita na bunge la Israel inaitaja "Israeli kama taifala Wayahudi wakati inatuma haki yake ya asili, utamaduni, dini, kihistoria," ikiongeza kuwa "haki ya kutumia uamuzi wa kujitawala katika taifa la Israeli imepewa tu Wayahudi ".

Serikali ya Uturuki ilikuwa tayari imekosoa wiki iliyopita sheria hiyo, ikiwashtumu viongozi wa Israeli kwamba inatafuta kuanzisha "taifa lenye ubaguzi wa rangi".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.