Pata taarifa kuu
ISRAELI-SYRIA-USALAMA

Jeshi la Israel lashambulia ngome za jeshi la Syria

Jeshi la Israeli limeendesha mashambulizi dhidi ya ngome za jeshi la Syria usiku wa kuamkia Alhamisi wiki hii katika mkjoa wa Qunitra karibu na Golan kwenye mpaka kati ya Israel na Syria, na kusababisha uharibifu mdogo, vyombo vya habari vya Syria vimearifu.

Askari wa Israeli karibu na mpaka wa Syria kwenye milima ya Golan, Februari 10, 2018.
Askari wa Israeli karibu na mpaka wa Syria kwenye milima ya Golan, Februari 10, 2018. REUTERS/ Ammar Awad
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Israeli, IDF (Tsahal), imetangaza kwamba imeendesha mashambulizi dhidi ya ngome tatu za jeshi la Syria kwa jibu la ndege isio na rubani ya Syria kuingia katika anga za Israel siku ya Jumatano.

Jeshi la Israeli "linaifahamisha serikali ya Syria kwamba linahusika na vitendo vilivyoendeshwa katika ardhi yake na linonya dhidi ya vitendo vingine dhidi ya majeshi ya Israeli," jeshi la Israel imesema katika taarifa yake.

Makombora yalirushwa na ndege za Israeli dhidi ya ngome kadhaa za jeshi, vyombo vya habari vya serikali ya Syria vimesema, vikinukuu chanzo cha kijeshi.

Angalau baadhi ya makombora yaliharibiwa na chombo cha ulinzi wa anga chaa Syria, vyombo vya habari vya serikali ya Syria vimeongeza.

Jeshi la Israel lilidungua ndege isio na rubani ya Syria siku ya Jumatano baada ya kuingia katika ardhi ya nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.