Jeshi la Israeli, IDF (Tsahal), imetangaza kwamba imeendesha mashambulizi dhidi ya ngome tatu za jeshi la Syria kwa jibu la ndege isio na rubani ya Syria kuingia katika anga za Israel siku ya Jumatano.
Jeshi la Israeli "linaifahamisha serikali ya Syria kwamba linahusika na vitendo vilivyoendeshwa katika ardhi yake na linonya dhidi ya vitendo vingine dhidi ya majeshi ya Israeli," jeshi la Israel imesema katika taarifa yake.
Makombora yalirushwa na ndege za Israeli dhidi ya ngome kadhaa za jeshi, vyombo vya habari vya serikali ya Syria vimesema, vikinukuu chanzo cha kijeshi.
Angalau baadhi ya makombora yaliharibiwa na chombo cha ulinzi wa anga chaa Syria, vyombo vya habari vya serikali ya Syria vimeongeza.
Jeshi la Israel lilidungua ndege isio na rubani ya Syria siku ya Jumatano baada ya kuingia katika ardhi ya nchi hiyo.