Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Watu zaidi ya kumi wauawa katika shambulizi Jalalabad

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga amejilipua Jumanne wiki hii katika mji wa Jalalabad, mashariki mwa Afghanistan, na kuua watu wasiopungua 10, kwa mujibu wa idara ya afya katika mji huo.

Mji wa Jalalabad unaendelea kukumbwa na mashambulizi ya washambuliaji wa kujitoa mhanga.
Mji wa Jalalabad unaendelea kukumbwa na mashambulizi ya washambuliaji wa kujitoa mhanga. REUTERS/Parwiz
Matangazo ya kibiashara

Mshambuliaji huyo amejilipua wakati alikuwa karibu na kituo cha mafuta, hali ambayo imesababisha moto mkubwa, na nyumba kadhaa kuteketea kwa moto.

Mlipuko huo pia umejeruhi watu wanne ambao wamesafirishwa hospitali, amesema Inamullah Miakhel, msemaji wa Idara ya Afya.

Nchi ya Afghanistan imeendelea kukabilia na mashambulizi ya hapa na pale, huku kundi la Taliban likinyooshewa kidole cha lawama kuhusika na mashambulizi hayo.

Hata hivyo hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na shambulizi hilo.

Mashambulizi hayo yamesababisha vifo vya watu wengi na wengine wengi kulazimika kuyahama makaazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.