Upinzani umeishtumu Urusi kwa kusababisha mazungumzo hayo kuvunjika baada ya kukataa pendekezo la kuondoka kwa wanajeshi wa Syria na wapiganaji wa Iran katika ngome zake.
Mapigano yameendelea kushuhudiwa nchini katika ngome za upinzani kama Deraa, Tafas na Saida na kusababisha vifo vya mamia ya raia katika siku za hivi karibuni.
Hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu alisema nchi yake imekubaliana na Urusi na vilevile Iran kuwe na ushirikiano wa karibu katika lengo la kutafuta amani ya kudumu huko Syria.