Pata taarifa kuu
SYRIA-USALAMA

Zaidi ya watu 20 wauawa katika mashambulizi Syria

Zaidi ya watu 20 wameuawa Alhamisi wiki hii katika mashambulizi yanayodaiwa kutekelezwa na ndege za kivita za Urusi dhidi ya mkoa wa Deraa nchini Syria. Haya ni mauaji ya watu wengi tangu kuanza kwa mashambulizi ya majeshi ya serikali na washirika wake kwa minajili ya kuwatimua waasi katika eneo hili muhimu.

Mkoa wa Deraa ulioshambuliwa na ndege za kivita za Urusi.
Mkoa wa Deraa ulioshambuliwa na ndege za kivita za Urusi. AFP
Matangazo ya kibiashara

Mataifa ya magharibi yamelaani operesheni za kijeshi zilizozinduliwa June 19 na utawala wa Bashar al-Assad na mshirika wake Urusi dhidi ya mkoa huu unaodhibitiwa kwa 70% na wapiganaji, na mashirika yasiyo ya kiserikali kadhaa yamesema yana wasiwasi ya kutokea mgogoro mpya wa kibinadamu katika nchi hii inayoendelea kukumbwa na vita tangu mwaka 2011.

Baada kuimarisha mamlaka yake katika mji mkuu Damascus na maeneo jiranie kwa kuwatimua waasi, utawala wa Assad ulianzisha mapigano mapya kusini mwa nchi, eneo muhimulinalopakana na Jordan na mlima mkubwa wa Golan, eneo linalodhibitiwa na Israeli.

Alhamisi wiki hii mashambulizi yaliyotekelezwa na ndege za Urusi yalilenga maeneo kadhaa mashariki na magharibi mwa mkoa wa Deraa, na kuua watu 22, kwa mujibu wa shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH).

Miongoni mwa waathirika, watu 17 ikiwa ni pamoja na watoto watano, waliokua walikimbilia katika handaki chini ya nyumba moja, kwa kuhofia usalama wao kutokana na mashambulizi wameuawa katika mashambulizi ya ndege za kivita za Urusi katika mji wa Al-Mseifra, OSDH imeeleza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.