Pata taarifa kuu
ISRAELI-SYRIA-USALAMA

Syria yashambuliwa kwa makombora kutoka Israeli

Makombora mawili ya Israeli yameanguka karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Damascus, nchini Syria, mapema Jumanne wiki hii, shirika la habari la Syria limearifu bila hata hivyo kutoa taarifa zaidi.

Ndege za Israeli ambazo zilitokea kwenye eneo lililo karibu na mlima wa Golan (kwenye mpaka na Syria) zilirusha makombora mawili karibu na uwanja wa ndege wa Damascus na kuharibu vifaa kadhaa vya jeshi la Syria.
Ndege za Israeli ambazo zilitokea kwenye eneo lililo karibu na mlima wa Golan (kwenye mpaka na Syria) zilirusha makombora mawili karibu na uwanja wa ndege wa Damascus na kuharibu vifaa kadhaa vya jeshi la Syria. REUTERS/Amir Cohen
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH) limesema kuwa mfumo wa ulinzi dhidi ya mashambulizi ya angani wa jeshi la Syria haukuweza kuzuia makombora hayo mawili.

Mlipuko mmoja ulisikika saa 01:00 usiku saa za Syria (sawa na saa sita usiku saa za Afrika ya Kati). Kwa mujibu wa chanzo cha kijeshi kutoka Israeli, ambacho hakikutaja jina, ndege za Israeli ambazo zilitokea kwenye eneo lililo karibu na mlima wa Golan zilirusha makombora mawili karibu na uwanja wa ndege wa Damascus na kuharibu vifaa kadhaa vya jeshi la Syria.

"Makombora hayo yalilenga ghala la silaha na vifaa vingine vya kijeshi na mabohari yanayomilikiwa na wanamgambo wasiokuwa wa Syria walio karibu na serikali," shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH) limesema, huku likiongezea kwamba halin ataarifa zaidi kuhusu hasara iliyosababishwa na mashambulizi hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.