Pata taarifa kuu
ISRAEL-UCHUMI

Mkewe Netanyahu ashtakiwa kwa ulaghai

Sara Netanyahu, mkewe Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anakabiliwa na mashitaka ya ulaghai kutokana na madai ya ubadhirifu wa fedha za umma. Hata hivyo Bi Netanyahu amekana kufanya makosa yoyote, akisema kuwa madai yasio kuwa na msingi kwa lengo la kuchafua jina lake tu

Waziri Mkuu wa Israel Benyamin Netanyahu na mkewe Sara Netanyahu, Mei 14, Jerusalem.
Waziri Mkuu wa Israel Benyamin Netanyahu na mkewe Sara Netanyahu, Mei 14, Jerusalem. REUTERS/Ronen Zvulun
Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya mwendesha mashtaka imesema imeamua kuwasilisha mashtaka dhidi ya wawili hao baada ya 'kuchunguza ushahidi wote na kupima uzito wa kesi yenyewe'.

Kwa mujibu wa mashtaka, Bi Netanyahu na bwana Seidoff wanatuhumiwa kwa kuhusika katika matumizi ya fedha kati ya Septemba 2010 na Machi 2013 walizotumia kununua chakula kilichopelekwa katika makaazi ya waziri mkuu na pia kuwaajiri wapishi binafsi.

Sara Netanyahu ameshtakiwa kwa ubadhirifu wa dola 100,000 kwa huduma za upishi katika makaazi rasmi ya waziri mkuu.

Wanasheria wake wamesema mteja wao hana hatia, huku wakiyataja mashtaka hayo kama ya kiwendawazimu na yasio na msingi wowote.

Wakati huo huo Waziri mkuu Netanyahu amejibu kwa hasira kwa kile ambacho kwa muda mrefu amekiona kuwa kuandamwa kwa familia yake na wanasiasa wa upinzani.

Hata hivyo upande wa mashitaka unasema una ushahidi wa kutosha kuwa Sara Netanyahu alihusika katika ulaghai huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.