Pata taarifa kuu
USALAMA-AFGHANSTAN-ASHRAF GHANI

Kundi la Taleban latangaza kusitisha mapigano kwa siku tatu

Kundi la Taleban nchini Afghanstani limetangaza kufikia makubaliano na serikali ya nchi hiyo ya kusitisha mapigano kwa siku tatu ili kupisha sikukuu ya Eid mwezi huu.

Rais wa Afghanstan, Ashraf Ghani
Rais wa Afghanstan, Ashraf Ghani DR
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo limekujaa saa chache baada ya kundi hilo kutekeleza mashambulizi yaliyopelekea kuuawa kwa askari 19 wa polisi nchini Afghanstan.

Rais wa Afghanstan Ashraf Ghan amesema hatua iliyochukuliwa na kundi la Taliban ni fursa kwa kundi hilo kutathimini kampeni zake za mashambulizi ambazo zinawatenganisha raia wa taifa hilo.

Hii ni mara ya kwanza kwa wanamgambo wa Taleban kutangaza kusitisha mapigano tangu mwaka 2001 ambapo Jeshi la Marekani lilipooongoza uvamizi nchini humo.

Hata hivyo kundi hilo,limesema halitaendesha mashambulizi yoyote wakati wa kipindi cha sikukuu isipokuwa kwa vikosi vya nje vilivyopo nchini Afghanstan.

Vikosi vya kigeni nchin i humo vimepunguzwa hadi kufikia 15,000 lakini rais wa Marekani Donald Trump, mwaka wa jana alitangaza kuwa vikosi vya Marekani nchini humo vitaendesha zaidi mashambulizi ya anga.

Sikukuu ya Eid-El-Fitr husherehekewa na waislamu duniani kote baada ya kutamatika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.