Pata taarifa kuu
ISRAEL-UFARANSA-IRAN-USHIRIKIANO

Waziri mkuu wa Israel azuru Ufaransa

Baada ya Ujerumani, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anafanya ziara ya kikazi Jumanne hii Juni 5 nchini Ufaransa, kabla ya kuelekea Uingereza siku ya Jumatano.

Waziri Mkuu wa Israel Benyamin Netanyahu wakati wa ziara yake Berlin Juni 4, 2018.
Waziri Mkuu wa Israel Benyamin Netanyahu wakati wa ziara yake Berlin Juni 4, 2018. REUTERS/Axel Schmidt
Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu wa Israel anataka kuzishawishi nchi hizi kujitoa kwenye mkataba wa nyuklia wa Iran, kama vile Marekani ilivyofanya. Netanyahu anataka kuitenga Iran, ambayo ni "tishio kubwa," kwa mujibu wa waziri huyo mkuu wa Israel.

Iran ni tishio kwa usalama wa Israel, amesisitiza Benjamin Netanyahu. Taarifa za hivi karibuni za Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, akiita Israel "saratani inayopaswa kukabiliwa," zinampa fursa zisizotarajiwa za kupitisha ujumbe wake ambao ni: "Hakuna kuzungumza tena na Tehran."

Iran haitaki tu kuwa na silaha ya atomiki lakini ushawishi wake katika kanda hiyo ni hatari, kwa mujibu wa Benjamin Netanyahu. "Wairan wanapaswa kuondoka Syria," alisema Benjamin Netanyahu, alipokua zirani mjini Berlin, siku ya Jumatatu, Juni 4. Wakati huo, mwenyeji wake Angela Merkel, alisisitiza juu ya uungwaji mkono wa Ujerumani kwa serikali ya Kiyahudi, mwandishi wetu mjini Berlin, Nathalie Versieux amearifu, kabla ya kukumbusha orodha ndefu ya tofauti kati ya Jerusalem na Berlin juu ya uchambuzi wa hali ya Mashariki ya Kati na njia za kufikia amani.

Nchi za Ulaya kwa sasa zinajaribu kuokoa mkataba wa nyuklia wa Iran, uliopata pigo kubwa kwa kujitoa kwa Marekani Mei 8. Kwa upande wa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, amesema kutetea mkataba huu ni njia pekee ya kuzuia Iran kupata silaha za nyuklia.

Emmanuel Macron yuko kwenye msimamo huo. Rais wa Ufaransa anatarajia kumpokea Benjamin Netanyahu Jumanne hii alaasiri. Ziara yake pia inakuja wiki tatu baada ya jeshi la Israel kuwafyatulia risasi waandamanaji wa Palestina huko Gaza na kuua watu 60 kwa siku moja, kitendo kilichotajwa na Emmanuel Macron kuwa ni cha "chuki". Mashirika mbalimbali yametoa wito wa kuandamana mjini Paris kupinga dhidi ya kuwasili kwa Waziri Mkuu wa Israel.

Hakuna sababu kwa Ufaransa, ambayo ni nchi ya haki za binadamu, kupokea kiongozi ambaye jeshi lake liliua watu wasio na silaha, wanawake na watoto, kwa kuwapiga risasi kwa mukusudi.

Dominique Pradalié, Katibu Mkuu wa chama cha Kitaifa cha Waandishi wa Habari, anasema ana wasiwasi juu ya kuja kwa Netanyahu nchini Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.