Pata taarifa kuu
ISRAELI-PALESTINA-HAMAS-USALAMA

Israel yaendesha mashambulizi dhidi ya ngome za Hamas

Jeshi la Israel limesema limeshambulia ngome 25 za wapiganaji wa Hamas katika ukanda wa Gaza. Israel imesema ilichukua hatua hii, baada ya Hamas kurusha kombora katika ardhi yake.

Ndege za kivita za Israel zikiendesha mashambulizi dhidi ya ngome za wapiganaji wa Hamas katika Ukanda wa Gaza, Mei 29, 2018.
Ndege za kivita za Israel zikiendesha mashambulizi dhidi ya ngome za wapiganaji wa Hamas katika Ukanda wa Gaza, Mei 29, 2018. REUTERS/Suhaib Salem
Matangazo ya kibiashara

Aidha, inaeleza kuwa, makombora 70 kutoka upande wa Palestina yalirushwa siku ya Jumanne kuwalenga raia wa Israel.

Mengi ya maroketi hayo yalidunguliwa na mitambo hiyo ya Iron Dome, kwa mujibu wa jeshi.

“Mitambo ya kudungua makombora ya Israel maarufu kama "Iron Dome anti-missile shield", imedungua roketi zilizovurumisha kutoka Ukanda wa Gaza baada ya ving’ora kulia kusini mwa Israel kuwaonya raia kukimbilia maeneo salama, “ jeshi la Israel limesem akatika taarifa yake.

Siku ya Jumatatu wanajeshi wa Israel walimua mwanamgambo wa Hamas na kuwakamata wengine wawili waliojaribu kuvuka mpaka kwenda Israel.

Takriban wapalestina 116 wameuawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa na wanajeshi wa Israel wakati wa maandamano na kuzua shutuma kali za kimataifa kutokana na mbinu ilizotumia Israel.

Israel inalaumu kundi la Hamas kwa kuchochea ghasia hizo madai kundi hilo linakana.

Wasiwasi umeendelea kushuhudiwa kati ya Israel na Palestina, baada ya Marekani kuhamishia Ubalozi wake mjini Jerusalem.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.