Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Watu 16 wauawa katika mlipuko wa bomu Kandahar

Watu wasiopungua 16 wameuawa na wengine 38 kujeruhiwa, wengi wao wakiwa raia wa kawaida Jumanne wiki hii katika mji wa Kandahar, mji mkuu wa kusini mwa Afghanistan. Tukio hilo metokea wakati vikosi vya usalama vilikua vikijaribu kutegua bomu lililokua limetegwa katika basi ndogo katikati mwa mji huo.  

Mmoja wa watu waliojeruhiwa akipewa huduma ya matibabu katika hospitali ya Kandahar Mei 22, 2018.
Mmoja wa watu waliojeruhiwa akipewa huduma ya matibabu katika hospitali ya Kandahar Mei 22, 2018. AFP
Matangazo ya kibiashara

Karibu saa nne baada ya mlipuko huo, uliotokea mchana, idadi ya watu waliopoteza maisha ilikua ikiongezeka, huku kukiwa na hatari ya waathirika kuendelea kukwama chini ya vifusi, afisa wa hospitali ya Kandahar ameonya.

"Nilikuwa katika duka langu wakati mlipuko ulipotokea, nilijikuta nikizingirwa na moshi, mkono sina (umekatika)," amesema mmoja wa waathirika akiliambia shirika la habari la AFP.

Kundi lililotaka kutumia gari hilo halijulikani na ilikua bado ni vigumu kujua kama shambulio lingelitekelezwa kwa wakati huo au lilikua limeandaliwa kwa tarehe ya baadaye.

Kwa mujibu wa mkuu wa polisi Mohammad Qasim Azad, akihojiwa na shirika la habari la AFP, "vikosi vya usalama tangu asubuhi vimekua katika operesheni ya kukamata magari ambayo yangeliweza kutumika kama katika mashambulizi ya kujitoa muhanga. Walikama basi ndogo iliyokua imejaa vilipuzi, ambyo ilikua iliegesha karibu na kituo cha basi ".

"Gari hilo lililipuka wakati ambapo polisi walikua wakijaribu kutegua vilipuzi hivyo," afisa huyo ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.