Pata taarifa kuu
ISRAELI-PALESTINA-HAMAS-USALAMA

Israeli yaishambulia Hamas, Jumuiya ya nchi za kiarabu yakutana

Vikosi vya ulinzi vya Israeli vimeendesha mashambulizi mapya dhidi ya ngome za Hamas katika Ukanda wa Gaza. Mashambulizi hayo yaliendeshwa Alhamisi wiki hii.

Askari wa Israeli wakipiga doria kando ya shamba linalotrketea kwa moto, upande wa Israeli kwenye mpaka kati ya Israeli na Gaza, Mei 14, 2018.
Askari wa Israeli wakipiga doria kando ya shamba linalotrketea kwa moto, upande wa Israeli kwenye mpaka kati ya Israeli na Gaza, Mei 14, 2018. REUTERS/Amir Cohen TPX IMAGES OF THE DAY
Matangazo ya kibiashara

Ndege za kijeshi za Israeli zimeshambulia ngome saba za Hamas katika Ukanda wa Gaza. Jeshi la Israeli limesema kuwa limelipiza kisasi kwa risasi zilizofyatuliwa zikiwalenga askari wake waliokua wamepiga kambi kando ya mpaka, lakini pia kwa risasi za bunduki ya kivita zilizozilizoangukia katika mji mgogo wa Sderot siku ya Jumatano .

Hali ya utulivuimerejea katika Ukanda wa Gaza baada ya vifo vya karibu Wapalestina 60 waliouawa siku ya Jumatatu wiki hii wakati wa maandamano na makabiliano yaliyoingiliana na sherehe ya ufunguzi wa ubalozi mpya wa Marekani katika mji wa Jerusalem.

Wakati huo huo Mawaziri wa kigeni wa kutoka nchi za Kiarabu wanakutana Alhamisi mchana mjini Cairo. Wataonyesha msimamo wao kuhusu "uchokozi wa Israel" dhidi ya Wapalestina na hatua ya Marekani ya kuhamisha ubalozi wake katika mji wa Jerusalem, kwa jumuiya ya nchi za Kiarabu, ambayo tayari imeomba uchunguzi wa Mahakama ya Kimataifa.

Uturuki itakua mwenyeji wa mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC), linalojumuisha nchi wanachama 57, kwa nia ya kutuma "ujumbe mzito kwa ulimwengu."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.