Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Mashariki ya Kati

Ubalozi wa Marekani Jerusalem: Raia wamiminika mitaani

media Mmoja wa Waandamanaji wa Palestina wakati wa maandamani dhidi ya hatua ya Marekani ya kuhamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem, Mei 14, 2018 katika Ukanda wa Gaza. REUTERS/Mohammed Salem

Makabiliano kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama vya Israel, yametokea Jumatatu wiki hii karibu na eneo linalotenganisha Palestina na Israel, baada ya marekani kutangaza kwamba itafungua rasmi ubalozi wake Jerusalem.

umatatu hii imetangazwa kuwa ni siku ya hasira kwa raia wa Palestina wakipinga hatua ya Marekani ya kuhamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem.

Maduka, shule na ofisi za serikali zinatarajiwa kufungwa katika Ukingo wa Magharibi, Ukanda wa Gaza na Jerusalemu ya Mashariki. Maandamano makubwa pia yamepangwa kufanyika Gaza. Makabiliano ya kwanza yalitokea na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa mapema Jumatatu hii asubuhi.

Kwa mwezi mmoaj na nusu, maandamano ya kila wiki yamekua yakifanyika kando ya eneo linalogawa Palestina na Israel. Maandamano hayo yamesababisha vifo vya watu 42 kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Kuna uwezekano wa kutokea machafuko makubwa Jumatatu hii mjini Jerusalem.

Kwa upande wa Israeli na Palestina, kunatarajiwa kuepo na maandamano makubwa katika Ukanda wa Gaza. Maandamano haya yanatazamiwa kuwa makubwa zaidi tangu kuanza kwa maandamano. Isreal imewatuma askari hadi 100,000 kando ya eneo hilo linalotenganisha mataifa hayo mawili.

Kwa upande wa waandaaji wa maandamano hayo wanasema, lengo ni kuvuka eneo linalotenganisha mataifa hayo mawili. Wanasema wataswali sala ya alasiri upande wa pili mpaka huo.

Kwa upande wa Israel, jeshi limetuma kikosi cha wanajeshi na magari ya kivita, vikosi maalum na maafisa wa upelelezi kwenye eneo linalotenganisha Palestina na Israel. Wameahidi kulinda uhuru wa taifa la Israeli na usalama wa wananchi wake. Na ndege zake zilirusha, siku ya Jumapili alasiri, vipeperushi vinavyowaonya wakazi wa Gaz kutothubutu kuvuka eneo linalotenganisha mataifa hayo mawili.

li kuepuka kutokea machafuko, Misri imejaribu kuleta upatanishi kwa kundi la Hamas. Kiongozi wa kundi hilo, Ismael Haniyeh alikua siku ya Jumapili nchini Misri. Lakini alirudi Gaza na amesema msimamo wao haujabadilika.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana