Pata taarifa kuu
PALESTINA-VENEZUELA-USHIRIKIANO

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas azuru Venezuela

Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, aliwasili siku ya Jumapili jioni nchini Venezuela ambapo anatarajiwa kukutana na mwenyeji wake Nicolas Maduro, ambaye anaunga mkono madai ya Palestina kwenye jumuiya kimataifa.

Kiongozi wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas.
Kiongozi wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas. REUTERS/Ammar Awad
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela, Jorge Arreaza alimpokea Bw. Abbas kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Maiquetia, karibu na Caracas. Kiongozi wa mamlaka ya Palestina anatarajia kupokelewa Jumatatu hii kwenye ikulu ya Miraflores ili kukutana na rais Maduro.

Ziara hii inakuja wakati ambapo Bw. Abbas alifutilia mbali shtuma za Israeli, Marekani, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa baada ya kutoa hotuba mbele ya baraza la Usalama la kitaifa nchini Palestina tarehe 30 Aprili, akionyesha kwamba mauaji yaliyotekelezwa dhidi ya Waisrael barani Ulaya, kupitia historia yake, yalisababishwa na ubaguzi wao katika jamii, hasa katika sekta ya benki.

Hata hivyo siku ya Ujumaa wiki iliyopita mahmoud abbas aliomba radhi kufuatia kauli yake hiyo na kulaani "ubaguzi na vitendo viovu vya kila aina".

Nicolas Maduro anatarajia kuwania muhula mwengine wakati wa uchaguzi wa urais wa Mei 20i, ambao utasusia na upinzani na ambao mfumo wake umeendelea kukosolewa kwa sehemu kubwa na jumuiya ya kimataifa.

Mnamo mwezi Januari, Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina, Riyad al-Malki alifanya ziara ya kikazi mjini Caracas, ambapo alipokea uungwaji mkono wa serikali ya venezuela dhidi ya uamuzi wa Washington wa kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israeli na kuhamisha ubalozi wake katika mji huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.