Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Watu 21 wauawa katika mashambulizi mawili Kabul

Watu 21 wameuawa na wengine 27 wamejeruhiwa katika mashambulizi mawili yaliyotokea katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Afghanistan.

Mashambulizi mawili yameuawa watu zaidi ya 20 katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul Aprili 30, 2018.
Mashambulizi mawili yameuawa watu zaidi ya 20 katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul Aprili 30, 2018. REUTERS/Omar Sobhani
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo mawili yalitokea kwa nyakati tofauti.

Shambulizi la kwanza liliendeshwa saa nane kabla na mtu aliyekua kwenye pikipiki. shambulio la pili liliendeshwa mtu mwengine dakika thelathini baada ya shambulio la kwanza.

Mshambuliaji wa pili alijilipua karibu na kundi la waandishi wa habari waliokua kwenye eneo la shambulio la kwanza. Mashambulio yote mawili yalitokea sehemu moja lakini kwa nyakati tofauti.

Kwa Kingereza

Shirika la habari la AFP limetangaza kifo cha Shah Marai, mmoja wa waandishi wake. Waandishi wengine watatu kutoka vituo vya televisheni vya Afghanistan wameuawa katika mashambulizi hayo. Wote walikua . Mashambulizi hayo yalitokea katikati mwa mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, karibu na ofisi ya usalama wa taifa (NDS).

Mpaka sasa hakuna mtu au kundi ambalo limedai kuhusika na mashambulizi haya, ambayo yanatokea wiki moja baada ya shambulizi la kujitoa mhanga katika kituo kimoja cha kujiandikisha kupiga kura mjini Kabul. Shambulizi ambalo liliua watu 60. Kundi la Taliban lilitangaza wiki moja iliyopita kwamba linaanza mashambulizi yake ya majira joto, na hivyo kufutilia mbali mazungumzo ya amani yaliyopendekezwa na serikali.

Kwa Kifaransa

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.