Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Mashariki ya Kati

Syria na washirika wake wajiandaa kwa mashambulizi ya Marekani

media Bendera za Syria na Hezbollah kwenye gari la kijeshi katika mkoa wa Qalamun ya magharibi, Syria, tarehe 28 Agosti 2017. REUTERS/Omar Sanadiki

Jeshi la Syria na washirika wake wamehama kutoka viwanja vya ndege na kambi za kijeshi nchini humo, pamoja na majengo ya Wizara ya Ulinzi na makao makuu ya jeshi Damascus, kwa kufuatia uwezekano wa mashambulizi ya Marekani.

Kufuatia uwezekano wa kutokea kwa mashambulizi ya Marekani nchini Syria, kundi la Hezbollah limewatuma saa 48 zilizopita wapiganaji wake walio nchini Syria tangu mwaka 2013 kupigana upande wa jeshi la Syria, vyanzo vya Libanon nchini Syria vimeiambia RFI.

Hezbollah ina wapiganaji kati ya 5,000 na 8,000 nchini Syria. Wanasaidia majeshi ya serikali ya Damascus, ikiwa ni pamoja na katika eneo la Ghouta mashariki, Aleppo, Quneitra, karibu Golan inayokaliwa na Israel, na katika mkoa wa mashariki wa Deir Ezzor. Kundi hili la Kishia limehamisha wapiganaji wake kutoka ngome kambi zake na limeanza zoezi la kuweka sawa wapiganaji wake, kwa mujibu wa vyanzo hivyo.

Kundi la Hezbollah na jeshi la Iran pia wamehamisha askari wao kutoka ngome zao katika viwanja vidogo vya ndege vya kijeshi vya al-Chaayrate na T4, katika mkoa wa Homs, ambapo kulikua kukihifadhiwa ndege zisizokuwa na rubani. Tarehe 9 Aprili uwanja wa ndege wa T4 ulishambuliwa kwa makombora, shambulizi ambalo liliua askari kadhaa wa Iran. Syria na Urusi walishtumu Israeli kuwa ilihusika na shambulizi hilo.

Hezbollah ilishiriki katika vita kabambe nchini Syria katika kipindi cha miaka minne iliyopita. Kwa mujibu wa mashahidi kundi hilo lilipoteza wapiganaji 2,000 na 5,000 waliojeruhiwa nchini humo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana