Pata taarifa kuu
SYRIA-USALAMA

Uwanja wa ndege wa kijeshi washambuliwa Syria

Watu wengi wameuawa katika mashambulizi dhidi ya uwanja wa ndege wa kijeshi nchini Syria. Mashambulizi hayo yanadaiwa kuwa yametekelezwa na meli za kivita, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali ya Syria la Sana.

Utawala wa Bashar Al Assad washtumiwa kutekeleza mashambulizi ya kemikali dhidi ya raia huko Duma, Aprili 8, 2018.
Utawala wa Bashar Al Assad washtumiwa kutekeleza mashambulizi ya kemikali dhidi ya raia huko Duma, Aprili 8, 2018. White Helmets/Reuters TV via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Shirika hili limesema "makombora kadhaa yalirushwa katika uwanja wa ndege wa Tayfur,karibu na mji wa Homs, mapema leo Jumatatu asubuhi.

Video moja ambayo imekuwa ikisambaa ambayo ilirekodiwa na wahudumu wa kujitolea wafahamikao kama White Helmets linawaonesha maiti za wanaume, wanawake na watoto kadha ndani ya jumba moja, maiti nyingi zikiwa na povu mdomoni.

Hata hivyo, imekuwa vigumu kubaini hasa nini kilitokea na idadi kamili ya waliofariki.

Mashambulizi haya katika uwanja wa ndege wa Tayfur, yanatokea wakati ambapo marais wa Marekani na Ufaransa, hivi karibuni walitangaza kwamba wanataka kutoa "jibu kali na la pamoja" baada ya "shambulio la kemikali" ambalo liliwaua watu wengi mashariki mwa Ghouta siku ya Jumamosi, Aprili 7. Kwa mujibu wa video zilizorushwa watumiaji wa Internet, mashambulizi hayo yalitekelezwa kutoka bahari ya Mediterranean.

Wakati huo huo makao makuu ya jeshi la Marekani Pentagon limefutilia mbali madai kuwa Marekani imehusika katika mashambulizi hayo. Pentagon imesema kuwa Marekani "haifanyi mashambulizi ya angani nchini Syria" hivi sasa. Hayo yanajiri wakati ambapo Rais wa Marekani Donald Trump anatarajia kukutana na uongozi wa jeshi la Marekani.

Siku ya Jumapili Rais wa Marekani Donald Trump alionya dhidi ya kile kinachoendelea kuwasibu raia wa Syria kufuatia mashambulizi ya kemikali yanayotekelezwa na utawala wa Bashar Al Assad, huku akionya kwamba yeye pamoja na washirika wake Iran na Urusi "watalipia sana".

Hata hivyo, inaonekana kwamba Trump sasa nataka kufanya kazi kwa ushirikiano na washirika wake wa magharibi, kwani alikuwa tayari alizungumza kwa simu na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Rais wa Ufaransa pia alionya kuwa utumiaji wa silaha za kemikali ni mstari mwekundu, ambao kuvukwa kwake itapelekea Ufaransa kuchukua majibu dhidi ya jeshi la Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.