Pata taarifa kuu
SYRIA

Syria: Wapiganaji zaidi kuondoka kwenye mji wa Ghouta

Kundi jipya la waasi nchini Syria pamoja na raia wanajiandaa kuondoka kwenye mji wa Ghouta Mashariki Jumatatu ya wiki hii siku chache baada ya kushuhudia mamia ya kundi jingine la waasi likiondoka kwenye mji huo ambao ulikuwa ngome ya waasi.

Mabasi yakiwa yanasubiri kuwabeba waasi wanaoondoka kwenye mji wa Ghouta, Syria. 24 Machi 2018.
Mabasi yakiwa yanasubiri kuwabeba waasi wanaoondoka kwenye mji wa Ghouta, Syria. 24 Machi 2018. REUTERS/Omar Sanadiki
Matangazo ya kibiashara

Majuma matano tangu vikosi vya Serikali vianzishe mashambulizi kwenye mji huo, kwa sasa wanaushikilia kwa zaidi ya asilimia 90 ya mji huo ulioko nje kidogo ya mji mkuu Damascus.

Maeneo mengi yameendelea mashambulizi makubwa ya mabomu na kuachwa ikiwa wazi kutokana na mamia ya watu kuondoka baada ya mazungumzo yaliyosimiwa na utawala wa Urusi.

Msafara wa wapiganaji 5400 na raia waliondoka kwenye maeneo ya mji wa Ghouta ambao ulikuwa unashikiliwa na wapiganaji wa kiislamu wa Faylaq al-Rahman siku ya Jumapili na kuelekea kaskazini mwa nchi ya Syria kwenye mji wa Idlib.

Idadi hii ilikuwa ni idadi kubwa ya kwanza kushuhudiwa katika siku moja kutoka mashariki mwa mji wa Ghouta baada ya watu 1000 kusafirishwa kwa mabasi kutoka kwenye mji huohuo siku ya Jumamosi.

Nchi ya Urusi ambayo ni washirika wakubwa wa Serikali wanashiriki kikamilifu katika kusimamia zoezi la wapiganaji hao kutoka kwenye mji wa Ghouta ambapo wamekuwa wakiwapakia wanajeshi wao waliojifunika nyuso kwenye mabasi hayo.

Watu zaidi wanatarajiwa kuondoka Jumatatu ya wiki hii kutoka kwenye maeneo ya Arbin na Zamalka na maeneo jirani ya Jobar maeneo yote haya yalikuwa yanakaliwa na kundi la Faylaq al-Rahman.

Msemaji wa kundi hilo Wael Alwan amethibitisha kuwa Jumatatu ya wiki hii watu zaidi wataondolewa kwenye maenei yanayoshambuliwa.

Mabasi zaidi yalikuwa tayari siku ya Jumatatu kuoakia watu zaidi ya 1000 wakiwemo wapiganaji, mamia ya watoto wote kutoka kwenye eneo moja, vyombo vya habari nchini Syria vimeripoti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.