Pata taarifa kuu
SYRIA

Waasi waanza kuondoka kwenye mji wa Ghouta chini ya makubaliano

Waasi wa Syria na familia zao wameanza kuondoka kwenye mji muhimu uliolengwa na mashambulizi mfululizo wa Ghouta mashariki ikiwa ni sehemu ya makubaliano na Serikali kuruhusu waondoke.

Baadhi ya raia wakiwa wanaondoka kwenye miji inayoshambuliwa nchini Syria hivi karibuni.
Baadhi ya raia wakiwa wanaondoka kwenye miji inayoshambuliwa nchini Syria hivi karibuni. REUTERS/Omar Sanadiki
Matangazo ya kibiashara

Kituo cha Serikali kimesema kuwa zaidi ya waasi 44 na raia 340 wameondoka kwenye mji wa Harasta.

Wapiganaji 1500 kutoka kundi la Ahrar al-Sham na raia 600 wanatarajiwa kusafirishwa kutoka Harasta kwenda kaskazini mwa mji wa Idlib.

Makubaliano ya kuondoka kwa waasi hawa ni ya kwanza tangu vikosi vinavyopigana sambamba na wanajeshi wa Serikali wazidishe mashambulizi kwenye mji wa Ghouta mwezi mmoja uliopita.

Waangalizi wa haki za binadamu wanasema kuwa jumla ya raia 1500 wamekufa kutokana na mashambulizi ya anga na roketi wakati wengine zaidi ya elfu 50 wamekimbia mji huo kutokana na mapigano.

Kuondoka kwa waasi hawa kumekuja baada ya wanajeshi na makundi mengine yenye silaha kushambulia vikosi vya waasi na kuwalazimisha kukimbia mbapo wamefanikiwa kuchukua asilimia 65 ya mji huo.

Televisheni ya taifa imeripoti pia raia 13 waliokuwa wanashikiliwa na waasi wameachia akiwemo mwanajeshi wa Serikali.

Makubaliano haya yalisimamiwa na Serikali pamoja na mshirika wake nchi ya Urusi na mapema Alhamisi asubuhi zoezi la kuwaondoa waasi hao lilianza.

Baadae kituo kimoja cha televisheni Sana kiliripoti kuwa jumla ya watu 384 wakiwemo waasi 44 waliruhusiwa kuondoka mji wa Harasta kwa kutumia mabasi kupitia maeneo yanayokaliwa na vikosi vya Serikali nje kidogo ya jiji la Damascus.

Ahrar al-Sham kundi ambalo linamiliki mji wa Harasta, limekubali kuweka silaha chini kwa kubadilishana na kuruhusiwa kwenda kwenye mji wa Idlib ambao ni ngome nyingine ya waasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.