Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Mashariki ya Kati

ICRC yataka kupelekwa kwa misaada ya haraka kwenye mji wa Afrin, Syria

media Wanajeshi wa Uturuki na wale wa jeshi huru la Syria wakiwa kwenye mji wa Afrin, Machi 18, 2018 Reuters/路透社

Mkurugenzi wa shirika la kimataifa la msalaba mwekundu juma hili ametoa wito wa kufikiwa kwa raia walioko kwenye mji wa Afrin nchini Syria ambao ulikuwa unakaliwa na wapiganaji wa Kikurdi, akisema wafanyakazi wa Uturuki hawaaminiki baada ya vikosi vya nchi hiyo kuuchukua mji huo.

Katika kile kinachoonekana ushindi mkubwa wa vikosi vya Uturuki katika vita vilivyodumu kwa miezi miwili kuwafurusha wapiganaji wa YPG kaskazini mwa Syria, vikosi hivyo vilifanikiwa kuingia kwenye mji huo pia ya upinzani ya kuchukua doria.

Peter Maurer rais wa kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu, amesisitiza uhitaji wa kuwasaidia raia waliobaki kwenye mji huo, akisema kuingia kwenye mji wa Afrin toka kuanza kwa operesheni hiyo imekuwa ni changamoto.

“Kutokana na mashambulizi ya sasa tunaidadi kubwa ya raia ambao hawana makazi,” Peter amewaambia wanahabari mjini Geneva baada ya ziara ya majuma mawili kwenye eneo la mashariki ya kati ikiwemo nchi ya Syria.

“Tunahitaji kupata njia ya haraka na nyepesei kwa raia hawa katika siku chache zijazo,” ambapo emeongeza kuwa ana matumaini kuwa hili litawezekana.

Muerer hata hivyo mbali na kutoa wito kwa mashirika ya misaada kufika kwenye mji huo, amesema wafanyakazi wa msalaba mwekundu kutoka Syria huenda wasiwe na wakati rahisi wa kufanya kazi na raia wa Kikurdi ambao vikosi vyao vimefurushwa.

Muerer ameongeza kuwa operesheni ya misaada kwenye mji wa Afrin itasalia kuwa ngumu kwa sasa.

Mwishoni mwa juma vikosi vya nchi ya Uturuki vilifanikiwa kuingia kwenye mji wa Afrika kaskazini mwa nchi ya Syria katika kile ilichosema ni vita dhidi ya makundi ya kijihadi ikiwemo kundi la YPG ambalo inasema ni kundi la kigaidi.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana