Pata taarifa kuu
SYRIA-URUSI-GHOUTA

Maelfu wakimbia ngome ya upinzani ya Ghouta nchini Syria

Maelfu ya raia wameukimbia mji wa Ghouta Mashariki nchini Syria baada ya mwezi mzima wa mfulululizo wa mashambulizi ya vikosi vya Serikali ambavyo vinakaribia kuudhibiti kabisa mji huo kutoka kwa waasi nje kidogo ya jiji la Damascus.

Hali ilivyo Mashariki mwa  Ghouta nchini Syria kutokana na mashambulizi yanayoendelea.Wakaazi wanakimbia.
Hali ilivyo Mashariki mwa Ghouta nchini Syria kutokana na mashambulizi yanayoendelea.Wakaazi wanakimbia. Abdulmonam Eassa/AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Bashar al-Assad ameendelea kujiimarisha madarakani wakati huu vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo vikiingia mwaka wa nane.

Assad ameendelea kusisitiza kuwa mashambulizi hayo yataendelea hadi pale ngome hiyo ya upinzani inayosalia itakapoangushwa.

Vikosi vya Assad vimefanikiwa pakubwa katika vita vya kuuchukua mji wa Ghouta ambao wakati fulani ulikuwa ngome kuu ya wapiganaji waasi.

Waangalizi wa masuala ya vita wanasema kuwa kwa sasa vikosi vya Syria vimefanikiwa kushikilia asilimia 70 ya mji huo na kuwagawa wapiganaji waasi katika makundi matatu ambayo hayana uwezo tena wa kukabiliana na vikosi vya Serikali na washirika wake nchi ya Urusi.

Waangalizi wa haki za binadamu wanasema idadi ya raia waliokimbia ndani ya siku moja kutoka kwenye mji huo ni kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya vita ya Syria.

Watu 350,000 wamepoteza maisha nchini Syria tangu mwaka 2011.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.