Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Mashariki ya Kati

Vita nchini Syria vimesababisha mauaji ya 350,000 tangu 2011

media Mashambulizi katika ngome ya upinzani Mashariki mwa Ghouta jijini Damacus mwezi Februari 2018 ©REUTERS/ Bassam Khabieh

Miaka saba ya mapigano nchini Syria kati ya wanajeshi wa serikali ya rais Bashar Al Assad na wapiganaji wa upinzani, yamesababisha vifo vya watu 350,000.

Takwimu hizi zimetolewa na Shirika ya Haki za Binadamu nchini Syria lenye makao yake jijini London nchini Uingereza.

Ripoti ya Shirika hiyo inaonesha kuwa jumla ya watu 353,935 wengi wao wakiwa ni raia wa kawaida ambao wameuawa tangu tarehe 15 mwezi Machi mwaka 2011, wakati mzozo wa Syria ulipoanza.

Vita vya Syria vinaingia mwaka wa nane kuanzia siku ya Alhamisi, wakati huu jeshi la Syria likiendeleza mashambulizi katika ngome ya upinzani ya Ghouta, nje kidogo ya jiji kuu Damascus.

Kati ya raia wa kawaida 106,390 waliopoteza maisha katika vita hivyo, 19,811 ni watoto huku 12,513 wakiwa wanawake.

Idadi ya wanajeshi wa serikali waliopoteza maisha ni 63,820 huku idadi ya wapiganaji wa upinzani waliangamia wakiwa ni 58,130.

Wengine waliouawa ni pamoja na wapigaji wa kundi la Islamic State, wapiganaji wa Kikurdi na makundi mengine ya kijihadi.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana