Kusikiliza Pakua Podcast
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
  Uchambuzi na makala 13/12 04h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
  Uchambuzi na makala 13/12 05h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
  Uchambuzi na makala 12/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
 • Ufaransa: Mmoja wa waandamanaji wanaovalia vizibao vya njao afariki baada ya kugongwa na lori Avignon
 • Raia wa pili wa Canada akamatwa nchini China
 • Uturuki: Watu wanne wapoteza maisha na 43 wajeruhiwa katika ajali ya treni Ankara (gavana)
 • Jerusalemu: Mshambuliaji avamia polisi wawili wa Israel kabla ya kuuawa (polisi)
 • DRC: Ghala la Tume ya Uchaguzi lateketea kwa moto siku kumi kabla ya uchaguzi (mamlaka)
Mashariki ya Kati

Idadi ya watu waliopoteza maisha Mashariki mwa Ghouta yafika 800

media KIkao kilichopita cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa REUTERS/Eduardo Munozrs

Mashambulizi ya jeshi la Syria katika ngome ya upinzani Mashariki mwa Ghouta, yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 800, kwa mujibu wa waangalizi wa mzozo huu.

Miongoni mwa watu waliopoteza maisha ni watoto 178, tangu kuanza kwa operesheni hiyo tarehe 18 mwezi Februari.

Takwimu hizi zimetolewa wakati huu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likitarajiwa kukutana kujadili mzozo huu hasa hatua ya Syria kukataa kusitisha vita kwa siku 30 kama ilivyoagizwa.

Urusi ambayo inaisaidia Syria, siku ya Jumanne ilipoteza raia wake 39 baada ya ndege ya abiria kuanguka katika kambi ya kijeshi nchini Syria.

Kuendelea kwa vita, kumesababisha mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu kutowafikia waathiriwa.

Mapema wiki hii, rais Bashar Al Assad alisema mapigano katika ngome hiyo ya upinzani inayosalia jijini Damascus, yataendelea hadi pale wapinza wake watakaposhindwa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana