Pata taarifa kuu
SYRIA-VITA-MISAADA YA KIBINADAMU

Vita Mashariki mwa Ghouta vyasitisha utoaji wa misaada ya kibinadamu

Mpango wa Mashirika ya Kimataifa ya kutoa misaada ya kibinadamu kuwafikia waathiriwa wa mzozo wa Ghouta Mashariki nchini Syria, umesitishwa baada ya kuzuka tena vita katika ngme hiyo ya upinzani.

Lori ilizobeba misaada ya kibinadamu nchini Syria.
Lori ilizobeba misaada ya kibinadamu nchini Syria. REUTERS/Omar Sanadiki
Matangazo ya kibiashara

Ndege za kivita za Syria zikisaidia na Urusi zilionekana angani na kurusha mabomu wakati misaada hiyo ya kibinadamu ikishushwa, hatua ambayo ilisababisha huduma hiyo kusitishwa.

Siku ya Jumatatu, watu 68 waliuawa wakati jeshi la Syria lilipotekeleza shambulizi katika ngome hiyo ya upinzani.

Tayari rais Bashar Al Assad amesema wanajeshi wake wataendelea kushambulia ngome hiyo ya upinzani.

Makabiliano hayo katika ngome hiyo ya upinzani inayosalia jijini Damascus kwa kipindi cha wiki nne zilizopita, yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 600 wasiokuwa na hatia.

Marekani, Ufaransa na Uingereza yameishtumu serikali ya Syria kwa kuendeleza vita licha ya kupitishwa kwa azimio la Umoja wa Mataifa, kutaka vita kukomeshwa kwa siku thelathini kuwaruhusu maelfu ya waathiriwa kupata misaada ya kibinadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.