sikiliza tena
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Mazungumzo ya amani kuanza Sudan, rais …
Rais wa DRC Felix Tshisekedi akiwa na mwenyeji wake rais wa Tanzania John Magufuli. 13 Juni 2019
 
Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/06 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/06 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/06 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Mashariki ya Kati

Umoja wa Mataifa kuchukua uamuzi kuhusu mapigano Syria

media Mapigano yaendelea kurindima Ghouta mashariki, Februari 21, 2018. REUTERS/Bassam Khabieh

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajia kukutana leo Ijumaa kupiga kura juu ya muswada wa azimio kuhusu usitishwaji wa mapigano kwa muda wa siku 30 nchini Syria.

Muswada huo unalenga kuruhusu kusafirishwa kwa misaada ya kibinadamu katika eneo la mapigano na kuwaondoa watu waliojeruhiwa na wagonjwa.

Tangazo hili lilitolewa na balozi wa Kuwait katika Umoja wa Mataifa, ambaye ni mwenyekiti wa mwezi huu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Mpaka sasa msimamo wa Urusi, mshirika wa Syria, haujulikani. Urusi ambaye ni mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa anaweza kutumia kura yake ya turufu, kwa kupinga azimio hilo.

Tangu kuanza kwa mgogoro nchini Syria, mgogoro ambao unaingia sasa mwaka wa nane, Urusi ambayo iliingia kijeshi nchini humo mnamo mwaka 2015 katika kusaidia vikosi vya Syria vinavyunga mkono serikali, imetumia kura yake ya turufu mara kumi na moja kupinga rasimu za maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa Syria.

Rasimu ya azimio inapaswa kupata kura tisa na sio kutokabiliwa na kura ya turufu kutoka kwa mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalam la Umoja wa Mataifa (Urusi, China, Marekani, Uingereza na Ufaransa).

Siku ya Alhamisi ndege za kivita ziliendesha mashambulizi katika eneo linaloshikiliwa na waasi Ghouta mashariki, karibu na Damascus, kwa siku tano mfululizo. Mashambulizi haya ya jana ni miongoni mwa mashambulizi mabaya tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa nchini Syria walitoa wito mapema mwezi Februari kusitishwa mapigano mara moja angalau kwa muda wa mwezi mmoja ili kusafirisha misaada ya kibinadamu katika maeneo ya mapigano.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana