Pata taarifa kuu
PALESTINA-UNSC-UTAMBUZI-USALAMA

Abbas aomba msaada wa kimataifa kwa Palestina

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas, ametangaza mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika "mkutano wa kimataifa" kwamba katikati ya mwaka 2018, itakua mwanzo wa "utaratibu wa kimataifa" kuunda taifa la Palestina.

Mahmoud Abbas katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, New York, 20 Februari 2018.
Mahmoud Abbas katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, New York, 20 Februari 2018. AFP
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa Mamlaka ya palestina ametoa msimamo wa nchi yake kwamba haikubaliani na Marekani kuwa msuluhishi katika mchakato wa amani katika Mashariki ya Kati, mchakatoa ambo umesimama kwa miaka kadhaa sasa.

"Ni muhimu kuanzisha utaratibu wa kimataifa kupitia mkutano wa kimataifa" ili kuleta amani Mashariki ya Kati, alisema Bw Abbas jana Jumanne katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, bila kufafanua wapi mkutano huo wa kimataifa utafanyika.

Mkutano huu utajumuisha Waisraeli na Wapalestina, wanachama watano wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,(Marekani, Urusi, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa) na nchi za kanda.

"Tusaidieni!", Aliomba rais wa Palestina kwa wanachama 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley amefutilia mbali hotuba ya kiongozi wa Mamlaka ya Palestina.

"Hatutakusaidia," alisema Nikki Haley, ambaye mnamo mwezi Januari alimshtumu kiongozi wa Palestina kukosa ujasiri.

Wakati wa hotuba yake mbele ya taasisi kuu ya Umoja wa Mataifa, rais wa Palestina aliomba nchi 55 ambazo hazitambua taifa la Palestina kwa jumla ya nchi 193 zinazounda Umoja wa Mataifa kuweza ulitambua.

"Tutarudi kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kuomba ulinzi huu" wa utambuzi kamili wa taifa la Palestina. "Kutambua taifa la Palestina hakuvurugi mazungumzo" bali kunachangia kuyaendeleza, Abbas alisisitiza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.