Pata taarifa kuu
SYRIA-USALAMA

Makubaliano kati ya jeshi la Syria na Wakurdi kukabiliana na Uturuki

Vyanzo vya serikali ya Syria, upinzani na vyama vya Kikurdi vinasema makubaliano yalifikiwa Februari 17 kati ya serikali ya Syria na vwanamgambo wa Kikurdi.

Wakurdi waandamana kwa kuunga mkno Wakurdi wa eneo la Afrin, kaskazini mwa Beyrtouh (Lebanon) Februari 5, 2018.
Wakurdi waandamana kwa kuunga mkno Wakurdi wa eneo la Afrin, kaskazini mwa Beyrtouh (Lebanon) Februari 5, 2018. JOSEPH EID / AFP
Matangazo ya kibiashara

Makubaliano hayo yanahusu kupelekwa kwa majeshi ya Syria katika eneo la Afrin ili kukabiliana na mashambulizi ya Uturuki.

Hata hivyo bado kuna mashaka kuhusu makubaliano hayo yanayoendelea kati ya Wakurdi na serikali ya Syria, pamoja na muda wa utekelezaji wake. Afisa wa ngazi ya juu katika wapiganaji wa kikurdi, Cheikho Bilo, alisema jana Jumapili kuwa jeshi la Syria linaweza kuanza kutumwa katika eneo la Afrin kuanzia leo Jumatatu Februari 19.

Taarifa hii haijathibitishwa na serikali ya Damascus , lakini vyanzo vivivyo karibu na serikali vinasema kuwa mazungumzo yamefikia kwenye hatua nzuri na inabakia tu kutatua masuala ya kiufundi.

Katika hali ya kutokwama kwa mazungumzo, pande mbili, zinazozungumza ambapo Urusi inashirki mazungumzo hayo, zimekubali kuahirisha maswala kuhusu usimamizi wa eneo la Afrin , ambao kwa sasa unashikiliwa na utawala uliyowekwa na wapiganaji wa Kikurdi.

Awali, mpango huo ulihusu kupelekwa kwa maelfu ya askari wa serikali ya Syria na wanamgambo wa serikali kwenye uwanja wa vitaili kukabiliana na jeshi la Uturuki na waasi wanaosadiwa na serikali ya Ankara. Askari wa Syria watakuja wakitokea mkoa jirani wa Aleppo. Wapiganaji wa Kikurdi wangeweza kutoa nafasi zao kwa askari wa serikali.

Kwa hatua ya pili, serikali ya Damascus ingelituma katika eneo la Afrin maafisa ambao watakaosimamia mambo ya utawala katika majengo ya umma na ya serikali, ambapo bendera rasmi ya Syria itapeperushwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.