Pata taarifa kuu
UN-SYRIA-VITA

Guterres ahofia mapigano yanayoendelea nchini Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kusitishwa kwa vita vinavyoendelea kushuhudiwa nchini Syria, hasa baada ya ndege za kivita za Israel kushambulia wanajeshi wa Iran na Syria.

Athari za mapigano katika eneo la Douma mjini Damascus, Syria, Februari 7, 2018
Athari za mapigano katika eneo la Douma mjini Damascus, Syria, Februari 7, 2018 REUTERS/ Bassam Khabieh
Matangazo ya kibiashara

Kupitia msemaji wake Stephane Dujarric , Guteress amesema ana wasiwasi kuwa iwapo mapigano hayatakoma, huenda yakasambaa hadi nje ya nchi ya Syria.

Aidha, ametoa wito kwa majeshi ya kigeni yaliyo nchini Syria kuheshimu sheria za Kimataifa na kutochokoza mataifa mengine.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema, mashambulizi ya angaa yaliyotekelezwa na jeshi la nchi yake nchini Syria, ni pigo kwa wanajeshi wa Syria na Iran.

Netanyahu ameongeza kuwa, jeshi la Israel litaendelea kukabiliana na maadui wake hasa wale wanaolenga kuwaumiza watu wake.

Aidha, amesisitiza kuwa, mashambulizi hayo yalilenga ngome za wanajeshi wa Syria na Iran, baada ya kudai kuwa ilichukua hatua hiyo baada ya ndege isiyokuwa na rubani ya Iran kuonekana katika angaa la Israel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.