Pata taarifa kuu
SYRIA-MAREKANI-USALAMA

Syria na matumizi ya silaha za kemikali dhidi ya waasi

Serikali ya Marekani imeituhumu Syria kutumia bomu zenye Kemikali zenye sumu katika mapambano yake dhidi ya ngome za waasi hapo jana mjini Douma ambao ni ngome ya waasi iliozingirwa na jeshi kaskazini mwa jiji la Damscus.

Serikali ya Syria inaendelea na mashambulizi ya anga katika mji wa Douma, eneo la waasi mashariki mwa Damascus, mji mkuu wa Syria.
Serikali ya Syria inaendelea na mashambulizi ya anga katika mji wa Douma, eneo la waasi mashariki mwa Damascus, mji mkuu wa Syria. AFP
Matangazo ya kibiashara

Mwishoni mwa mwezi Octoba mwaka jana wataalamu wa Umoja wa Mataifa waliishtumu moja kwa moja serikali ya Syria kutumia silaha za kemikali katika kambi ya Khan Sheikhun

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa walifahamisha kuwa utawala wa Syria ulitumia gesi yenye sumu katika shambulizi liliotekelezwa katika kijiji cha Khan Sheikhun Kaskazini mwa Syria.

Shambulizi hilo lilisababisha vifo vya watu zaidi ya 100 na kuwajeruhi wengine 500.

Shambulizi hilo lilitekelezwa mnamo mwezi Aprili mwaka 2017.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa ni kwamba ripoti ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu silaha zilizopigwa marufuku walifahamisha kuwa uchunguzi ulionesha kuwa  ndege ya kivita ya serikali ya Assad ilishambulia kijiji hicho kwa mabomu ya kemikali.

Syria na mshirika wake Urusi wameendelea kukana kuhusika na shambulizi lolote la kemikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.