Pata taarifa kuu
MAREKANI-SYRIA-UHAMIAJI

Utawala wa Trump waruhusu maelfu ya wakimbizi kutoka Syria kuishi Marekani

Utawala wa Donald Trump umewaruhusu karibu wakimbizi 7,000 kutoka Syria wanaoishi nchini Marekani kuendelea kuishi nchini humo kwa muda wakati vita vikiendelea nchini mwao.

Kambi ya Bab al-Salama, karibu na mpaka na Uturuki, Februari 6, 2016. Kati ya wahamiaji milioni 4.6 wa Syria walioorodheshwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR), zaidi ya nusu (2.7 milioni) wanapewa hifadhi Uturuki.
Kambi ya Bab al-Salama, karibu na mpaka na Uturuki, Februari 6, 2016. Kati ya wahamiaji milioni 4.6 wa Syria walioorodheshwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR), zaidi ya nusu (2.7 milioni) wanapewa hifadhi Uturuki. AFP/Bulent Kilic
Matangazo ya kibiashara

Mpango wa hadhi ya ulinzi kwa raia wa Syria ulipangwa kufikia kikomo tarehe 31 Machi.

"Tutaendelea kuchunguza maombi ya kila nchi kwa kuzingatia hali ya nchi husika. Kwa raia wa Syria ambao tayari wanaishi na kufanyia kazi nchini Marekani, mpango wa TPS utarefushwa kwa miezi mingine 18. Lakini Wasyria walioingia nchini Marekani baada ya Agosti 2016 watatengwa na mpango huo licha ya kuendelea kwa hali mbaya nyumbani, " amesema Waziri wa Usalama wa Ndani Kirstjen M Nielsen katika taarifa yake.

Wakambizi hao Walikuwa wakiishi nchini Marekani kwa muda dhidi , huku wakipewa kinga ya kutorejeshwa nyumbani chini ya mpango unaofahamika kama “Temporary Protected Status (TPS).”

Mapema mwaka huu, Wizara ya Usalama wa Ndani ilitangaza kuwa itafikisha kikomo mpango wa kinga kwa raia 262,500 kutoka El Salvador, ingawa hatua hiyo itacheleweshwa kwa miezi 18.

Mwezi Novemba, utawala huo ulisema kuwa hadhi ya ukimbizi ya raia takriban 59,000 wa Haiti itakwisha 2019.

Hivi karibuni Rais Trump alisema kuwa Wakimbizi wanatishia usalama wa Marekani. Hata hivyo amefuta mpango wa kibinadamu (TPS) kwa nchi mbali mbali katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni. Hatua hiyo tayari imewaathiri wahamiaji kutoka nchi mbalimbali kama vile Nicaragua, El Salvador na Haiti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.