Mlipuko waua watu wanane Pakistan
Watu wanane wameuawa leo Jumanne katika mlipuko wa bomu iliyotegwa kando ya barabara kaskazini-magharibi mwa Pakistani, shambulio ambalo linaonekana kuwa limekua limelenga jamii ya Mashia.
Imechapishwa:
Bomu hilo lililipuka katika wilaya ya Maqbal kwenye mpaka na Afghanistan, wakati ambpo basi dogo lililokua likisafiri na watu tisa lilipokua likipita.
Watu 8, ikiwa ni pamoja na wanawake watatu na mvulana mwenye umri wa miaka saba, wameuawa, kwa mujibu wa afisa mkuu wa eneo hilo, Basir Khan Wazir.
Ni vigumu kutambua miili yawatu waliouawa, lakini wote wanaonekana kuwa ni Waislamu kutoka jamii ya Mashia, afisa mmoja aliliambia shirika la habari la AFP. Afisa wa idara ya ujasusi katika eneo hilo amethibitisha shambulio hilo na idadi ya watu waliouawa
Eneo la Kurram limekua likikumbwa na mashambulizi ya hapa na pale, mashambulizi ambayo yamekua yakiwalenga watu kutoka jamii ya Mashia.