Pata taarifa kuu
PAKISTAN-USALAMA

Mlipuko waua watu wanane Pakistan

Watu wanane wameuawa leo Jumanne katika mlipuko wa bomu iliyotegwa kando ya barabara kaskazini-magharibi mwa Pakistani, shambulio ambalo linaonekana kuwa limekua limelenga jamii ya Mashia.

Nchi ya Pakista imeendelea kukabiliwa na visa vya mauaji. Hapa mmoja wa wahalkifu akamatwa na polisi
Nchi ya Pakista imeendelea kukabiliwa na visa vya mauaji. Hapa mmoja wa wahalkifu akamatwa na polisi REUTERS/Naseer Ahmed
Matangazo ya kibiashara

Bomu hilo lililipuka katika wilaya ya Maqbal kwenye mpaka na Afghanistan, wakati ambpo basi dogo lililokua likisafiri na watu tisa lilipokua likipita.

Watu 8, ikiwa ni pamoja na wanawake watatu na mvulana mwenye umri wa miaka saba, wameuawa, kwa mujibu wa afisa mkuu wa eneo hilo, Basir Khan Wazir.

Ni vigumu kutambua miili yawatu waliouawa, lakini wote wanaonekana kuwa ni Waislamu kutoka jamii ya Mashia, afisa mmoja aliliambia shirika la habari la AFP. Afisa wa idara ya ujasusi katika eneo hilo amethibitisha shambulio hilo na idadi ya watu waliouawa

Eneo la Kurram limekua likikumbwa na mashambulizi ya hapa na pale, mashambulizi ambayo yamekua yakiwalenga watu kutoka jamii ya Mashia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.