Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Mashariki ya Kati

Pence: Ubalozi wa Marekani kuhamia Jerusalem mwaka 2019

media Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence akikutana kwa mazungumzo na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, Jumatatu Januari 22, 2018. /REUTERS/Ariel Schalit

Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence ametangaza leo Jumatatu kuwa ubalozi wa Marekani utahamishiwa Jerusalem, "mji mkuu wa Israeli", mwaka ujao, wakati wa ziara yake ambapo hatakutana na viongozi wa Palestina ambao wamesusia ziara yake.

Katika hotuba yake kwa bunge la Israeli, Knesset, Mike Pence ametangaza zoezi la kuhamishia ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem litafanyika kabla ya mwisho wa mwaka 2019.

"Katika wiki zijazo, utawala wetu utaonesha mpango wake wa kufungua ubalozi wa Marekani Jerusalem - na utafungua kabla ya mwisho wa mwaka ujao," Bw Pence amesema.

"Jerusalem ni mji mkuu wa Israeli na, kwa hali yoyote ile, Rais Trump ameagiza wizara ya mashauriano ya kigeni kuanza maandalizi ya kuhamisha Ubalozi wetu kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem," Makamu wa Rais wa Marekani amesema, bila hata hivyo kutoa tarehe maalum.

Wabunge wa Israeli wenye asili ya Kiarabu ambao walikua wamepinga dhidi ya msimamo wa Marekani, kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa taifa la Israeli, walifukuzwa kutoka bunge la nchi hiyo, Knesset.

Akiwasili nchini Israeli usiku wa Jumapili akitokea Jordan baada ya zaira yake Jumamosi jioni nchini Misri, Mike Pence alipokea na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Alisema atafurahi kuwa "katika mji mkuu wa Israel, Jerusalem", huku Benjamin Netanyahu akijibu: "Hii ni mara ya kwanza mimi hapa katika hali ambapo viongozi wawili wanaweza kusema maneno matatu: Jerusalemu, mji mkuu wa Israeli".

Tangazo la Donald Trump mwezi uliopita liliwakasirisha Wapalestina, ambao waliamua kususia ziara ya Mike Pence, huku washirika wengi wa Marekani kutoka Ulaya wakiwa na wasiwasi.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana