Pata taarifa kuu
UTURUKI-SYRIA-KURDI

Jeshi la Uturuki laendeleza mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi nchini Syria

Uturuki imetuma wanajeshi wake Kaskazini mwa Syria katika operesheni ya kupambana na wapiganaji wa Kikurdi wanaopambana na kundi la Islamic State.

Jeshi la Uturuki likiingia nchini Syria
Jeshi la Uturuki likiingia nchini Syria REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Uturuki inasema wapiganaji hao ni magaidi na ni hatari kwa usalama wa nchi yake na ni lazima waondolewe kabisa.

Wapiganaji hao wanaofahamika kama YPG, ngome yao kuu ni Afrin nchini Syria mpakani na Uturuki.

Ripoti zinasema kuwa kumeshuhudia makabiliano makali kati ya wanajeshi wa Uturuki na wapiganaji hao, huku kukiwa na wasiwasi wa kutokea kwa maafa makubwa.

Uamuzi huu wa Uturuki huenda ukazua mgogoro kati yake na Marekani ambao inawaunga mkono wapiganaji hao kwa kile inachosema inasaidia katika vita dhidi ya Islamic State nchini Syria.

Serikali ya Syria inasema Uturuki haikuwaambia kuhusu, operesheni hii licha ya serikali ya Ankara kusema kuwa ikuwa imeiambia serikali ya Damascus.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.