Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 07/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 08/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 08/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Mashariki ya Kati

Marekani yasitisha msaada wa fedha kwa Palestina

media «Palestina, taifa la 194 la Umoja wa Mataifa, "raia huyu ampongeza Mahmoud Abbas, ambaye aliombataifa la Palestina kutambuliwa na kujiunga na Umoja wa Mataifa mnamo mwezi Septemba 2011. Reuters/Sharif Karim

Marekani imesitisha msaada kwa taifa la Palestina unaokadiriwa kuwa sawa na zaidi ya nusu ya fedha zake ilizokuwa ikizitoa kusaidia Wapalestina.

Marekani imekuwa ikitoa karibu asilimia 30 ya bajeti yake, kutoa huduma za afya, elimu na huduma za jamii.

Marekani inasema itazuia dola milioni 65 kwa ''kufikiria mustakabali ujao''. Lakini kabla ya hapo itatuma kiasi cha dola milioni 60 ya malipo yake ya kwanza ya mwaka huu.

Hivi karibuni rais Donald Trump alitishia kukata msaada iwapo Wapalestina wataendelea kupinga juhudi za amani na Israel.

Kwa upande wake Afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa amesema hatua hiyo ita haribu matokeo mazuri ya maelfu ya Wapalestina wasio na maisha bora yenye usalama.

Wakati huo huo Palestina imesema uamuzi wa Marekani unathibitisha kwamba nchi hiyo inaendelea kuangamiza haki za Wapalestina.

Siku ya Jumapili Januari 14 rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas alimshutumu rais Donald Trump kuvuruga juhudi za kupatikana kwa amani Mashariki ya kati.

Palestina na nchi kadhaa za Kiarabu zimeendelea kupinga Marekani katika kutafutia ufumbuzi mgogori wa Mashariki ya Kati kati ya Israel na Palestina, baada ya rais trump kuchukua hatua ya kutambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana