Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 07/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 08/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 08/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Mashariki ya Kati

Palestina: Tumeanzisha mchakato wa kutoitambua Israel

media Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas katika kikao cha Halmashauri Kuu ya PLO Januari 14, 2018 Ramallah. REUTERS/Mohamad Torokman

Viongozi wa Palestina wamesema wanataka kutoitambua Israel. Hatua ambayo inakuja baada ya Marekani kuchukua hatua ya kutambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.

Iwapo hili litafanyika, uhusiano kati yake na Isreal utaendelea kuwa mbaya zaidi.

Wakuu wa Palestina katika mkutano wao wakiongozwa na rais Mahmoud Abbas, wamesema hatua hiyo itachukuliwa kutokana na hatua ya Marekani kutambua Jerusalem kuwa Makao makuu ya Israel.

Mwishoni mwa juma lililopita Kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas alimshutumu rais wa Marekani Donald Trump, na kusema Palestina haiwezi kukubali kamwe Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Abbas, alisisitiza kuwa Jerusalem ni makao makuu ya kisiasa, kiimani ya Palestina na kumkejeli rais Trump kwa kubadilisha ramani hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Hivi karibuni Marekani ilitishia kufunga misaada yake kwa Palestina, huku Palestina ikisema haitakubali kutumiwa na Marekani kutokana na misaada yake. Marekani imekuwa ikitoa msaada wa kifedha kwa Palestina kusaidia kuimarisha usalama.

Wachambuzi wa siasa za eneo la Mashariki ya Kati, wanasema kuwa, tishio hili la Marekani ni kujaribu kuilazimisha Palestina kuja katika meza ya mazungumzo na Israel.

Marekani imekuwa ikitoa msaada huo wa kifedha kusaidia kuimarisha usalama lakini pia, kuendeleza maendeleo mbalimbali ya kiuchumi.

Palestina imekuwa ikisema kuwa Marekani kwa kutoa tangazo hilo, haiwezi kuwa msuluhushi anaependelea upande mmoja katika harakati za kutafuta suluhu ya mzozo kati yake na Israel.

Uhusiano kati ya Marekani na Palestina, umedorora baada ya rais Trump, kutangaza kutambua mji wa Jerusalem kuwa makao makuu ya Israel.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana