Pata taarifa kuu
IRAN-MAREKANI-EU

Marekani yataka mazungumzo zaidi kuhusu mkataba wa nyuklia nchini Iran

Rais wa Marekani Donald Trump amesema nchi yake inasitisha vikwazo dhidi ya Iran kwa mara ya mwisho, ili kutoa nafasi kwa bara la Ulaya na Marekani kuthathmini upya mkataba kuhusu mradi wa nyuklia wa Iran.

Mohammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya nje wa Iran
Mohammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya nje wa Iran REUTERSAlexander Zemlianichenko/Pool
Matangazo ya kibiashara

Hii inamaanisha kuwa, Iran haitashuhudia vikwazo vyovyote kutoka kwa Marekani kwa muda wa siku 120 zijazo.

Rais Trump amekuwa akishtumu mkataba ulioafikiwa kati ya Mataifa ya Magharibi na Iran, kusitisha mradi huo hadi mwaka 2025, kuwa mbovu.

Badala yake, Trump anataka mkataba huo kuangaliwa upya na kurekebishwa kwa lengo la kuizua kaboa Iran kuendelea na mradi huo.

Msimamo wa Marekani unaungwa mkono na Israel ambayo imeendelea kuamini kuwa mradi huo wa nyuklia wa Iran, unalenga kuishambulia kutumia silaha za maangamizi.

Iran kupitia Waziri wake wa Mambo ya nje Mohammad Javad Zarif amesema Marekani kuendelea na vitisho hivyo ni ishara ya kutotaka kutekelezwa kwa mkataba huo.

Mataifa ya Ulaya yakiongozwa na Ufaransa, Uingereza na Ujerumani yamemtaka rais Trump kukubali kutekelezwa kwa mkataba huo.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.