SYRIA-MAZUNGUMZO-SIASA
Upinzani Syria wataka Marekani kuingilia kati mazungumzo
Upinzani nchini Syria, inasema itazungumza na Marekani ili kuingilia kati mazungumzo ya amani yanaoongozwa na Umoja wa Ulaya.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Mjumbe wa upinzani katika mazungumzo hayo amesema, upinzani hautaki Urusi kuonekana kuwa mstari wa mbele kuongoza mazungumzo hayo.
Wito huu wa upinzani unakuja kuelekea mazungumzo mapya, yanayotarajiwa kuanza tarehe 21 mwezi huu jijini Genva nchini Uswisi.
Hadi sasa mazungumzo yote yaliyofanyika, hayajazaa matunda.
Mchafuko nchi Syria yamesababisha maelfu ya watu kuuawa na wengine kuyahama makazi yao.