Pata taarifa kuu
SYRIA-USALAMA

Mlipuko katika makao makuu ya wanajihadi wasababisha vifo vya watu 23

Mlipuko ambao chanzo chake hakijulikani katika makao makuu ya wapiganaji wa Kiislamu barani Asia katika mji wa Idlib, kaskazini magharibi mwa Syria, umeua watu 23, ikiwa ni pamoja na raia saba, kwa mujibu wa shirika la Haki za Binadamu nchini humo (OSDH ).

Mashambulizi yanaedelea katika jimbo la Idlib, Syria
Mashambulizi yanaedelea katika jimbo la Idlib, Syria REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Wapiganaji kutoka nchi za Asia, hususan Asia ya Kati, pamoja na watu kutoka jamii ya Uyghurs kutoka mkoa wa China wa Xinjiang, ni sehemu ya makundi ya wapiganaji wa Kiislamu nchini Syria.

"Mlipuko mkali ulitokea katika makao makuu ya wapiganaji hao katika mji wa Idleb, na kuua watu 23, ikiwa ni pamoja na raia saba," mkurugenzi wa OSDH, Rami Abdel Rahman, ameliambia shirika la habari la AFP, bila taja idadi ya watu waliojeruhiwa.

Watu wengi pia walijeruhiwa katika mlipuko huo, wengi ni wapiganaji, Abdel Rahman amesema, akiongeza kuwa makao makuu ya "askari wa Caucasia" yameharibiwa kabisa, na majengo yaliyo karibu yaliharibiwa sana.

OSDH, ambayo ina mitandao mikubwa ya vyanzo nchini Syria, hakueleza kama mlipuko huo ulisababishwa na bomu lililotegwa katika gari au ndege isio na rubani ya muungano kimataifa dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu au ndege ya Urusi, mshiriki wa utawala wa Bashar Al Assad.

Ripoti zinasema kuwa, kambi hiyo imekuwa ikiwahifadhi Majihadi ambao wamesajiliwa kutoka mataifa kadhaa ya bara Asia.

Haijahamika chanzo cha mlipuko huo lakini, mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema kuwa, kuna uwezekano mkubwa kuwa bomu hilo lilitengwa ndani ya gari dogo.

Lakini kwenye mitandao ya kijamii, watu kadhaa wamesema mlipuko huo umesababishwa na bomu lililotegwa katika gari.

Kundi la "Askari wa Caucasus" linajumuisha mamia ya wapiganaji kutoka Asia ya Kati, wapiganaji wa kundi la Tahrir al-Sham na wapiganaji kutoka nchi mbalimbali za bara la Asia.

Tangu mwishoni mwa mwezi Desemba, kusini-mashariki ya jimbo hili, linalodhibitiwa na kundi la Tahrir al-Sham - limekuwa eneo la mapigano makubwa kati ya serikali ya Syria na mshirika wake Urusi kwa upande mmoja, na makundi ya waasi kutoka kusini mwa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.