Pata taarifa kuu
ISRAEL-KRISMASI-DINI

Wakristo duniani washerehekea Sikukuu ya Krismasi

Shamrashamra za Krismasi zinaendelea kote duniani Jumatatu hii, siku ambayo Wakiristo wanasherehekea sikukuu ya kuzaliwa kwa Mwokozi wao Yesu Kristo.

Hivyo ndivyo Wakristo wanasherehekea Sikukuu a Kirismasi Hamburg, Ujerumani.
Hivyo ndivyo Wakristo wanasherehekea Sikukuu a Kirismasi Hamburg, Ujerumani. Daniel Reinhardt / dpa / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakiristo wanaamini kuwa kuzaliwa kwa Yesu Kristo kuliwaletea ukombozi.

Tarehe 25 mwezi Desemba kila mwaka, Wakiristo kote duniani hutumia siku hiyo kwenda Makanisani na baadaye kusherehekea pamoja  nyumbani na maeneo mengine kwa kula vyakula na kutoa zawadi.

Mjini Bethlehem nchini Israel, mji ambao Wakiristo wanaamini kuwa Yesu alizaliwa, mwaka huu shamrashamra zinashuhudiwa  lakini sio kwa kiasi kikubwa.

Wasiwasi unashuhudiwa na watalii wengi, hawajakwenda katika mji huo kwa kuhofia usalama wao.

Hatua hii inakuja baada ya Marekani hivi karibuni, kutambua mji wa Jerusalem kama makao makuu ya Israel hatua ambayo imeikasirisha Palestina na mataifa ya Kiislamu na yale ya Kiarabu.

Wiki hii, kulikuwa na mkutano wa dharura wa Umoja wa Mataifa kulaani hatua hiyo ya Marekani.

Kumeendelea kushuhudiwa makabiliano kati ya waandamanaji wa Kipalestina na wanajeshi wa Israel na kufikia siku ya Jumapili, rais wa Palestina 12 walipoteza maisha.

Uamuzi wa Marekani, umeelezwa na washirika wa Palestina kuwa, umehatarisha uwezekano wa kupatikana kwa amani kati yake na Israel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.