Pata taarifa kuu
GUATEMALA-ISRAELI-USHIRIKIANO

Guatemala yatangaza kuhamishia ubalozi wake Jerusalem

Rais wa Guatemala Jimmy Morales, ametangaza nia yake ya kuhamisha ubalozi wa nchi yake nchini Israeli katika mji wa Jerusalem. Baada ya Marekani, nchi hii ndogo katika kanda ya Amerika ya Kati ni taifa la kwanza kuamua kuhamisha ubalozi wake katika mji tata wa Jerusalem.

Mji wa Jerusalem, Desemba 4, 2017.
Mji wa Jerusalem, Desemba 4, 2017. ©EUTERS/Ronen Zvulun
Matangazo ya kibiashara

Katika kutaka kuhamisha ubalozi wa Guatemala kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem, rais Jimmy Morales amefuata msimamo wa Donald Trump na kuonyesha mafungamano yake na Washington, hata kama ameeleza kwamba uamuzi wake unatokana na uhusiano mzuri wa nchi yake na Israeli.

Rais Morales pia alisema kuwa alikutana kwa mazungumzo siku ya Jumapili Desemba 24 na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, ambayo amfahamisha uamuzi wake.

Tangazo hili halikuwashangaza wengi, kwa sababu Guatemala ni moja kati ya nchi tisa zilizounga mkono Marekani na Israeli wakati wa kura ya Alhamisi, Desemba 21, kuhusu azimio la Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Azimio hilo lilishtumu uamuzi wa Marekani kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa taifa la Kiyahudi.

Siku moja kabla ya mkutano huo rais Donald Trump alitishia nchi ambazo zitapigia kura azimio kuwachukulia vikwazo vya kifedha kutoka Marekani. Kwa sababu Guatemala inategemea kwa kiasi kikubwa msaada wa kiuchumi kutoka Marekani. Ni wazi kuwa rais Jimmy Morales amekubali kufanya hivyo shinikizo kutoka ikulu ya White House.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.