Pata taarifa kuu
YEMEN-SAUDI ARABIA

Saudi Arabia: Waasi wa Yemen warusha kombora jingine kulenga makazi ya mfalme

Muungano wa nchi washirika zinazoongozwa na Saudi Arabia katika vita dhidi ya waasi wa Huthi nchini Yemen, umesema wamefanikiwa kuzuia shambulizi la roketi iliyorushwa na waasi hao jirani na mji mkuu Riyadh.

Moja ya roketi ambazo hivi karibuni Saudi Arabia ilidai kuidungua baada ya kurushwa na waasi wa Houthi wa Yemen
Moja ya roketi ambazo hivi karibuni Saudi Arabia ilidai kuidungua baada ya kurushwa na waasi wa Houthi wa Yemen REUTERS/Ronen Zvulun
Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya walioshuhudia kudunguliwa kwa roketi hiyo wamechapisha picha za video kwenye mtandao zikionesha moshi angani baada ya mitambo maalumu ya Saudi Arabia kufanikiwa kudungua roketi hiyo kabla ya kufika aridhini.

Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi kuroka kwa Serikali ya Saudi Arabia kueleza ikiwa mashamblizi haya ya roketi yamesababisha madhara yoyote.

Kituo cha televisheni cha vuguvugu la waasi hao al-Masirah TV kimethibitisha waasi hao kurusha roketi aina ya Burkan 2 kulenga makazi ya kifalme ya al-Yamama.

Mwezi waaasi hao walirusha kombora jingine lililokuwa lilenge uwanja wa ndege wa Riyadh.

Saudi Arabia na Marekani zimeituhumu nchi ya Iran kwa kuwasaidia waasi hao wa Yemen kwa roketi.

Hata hivyo nchi ya Iran imekanusha tuhuma kuwa inawasaidia waasi wa vuguvugu la Houthi, ambao wamekuwa wakipigana dhidi ya Serikali na muungano unaoongozwa na Saudi Arabia tangu mwaka 2015.

Kituo cha televisheni cha al-Masirah kimechapisha kwenye ukurasa wake kikionesha makamanda wa waasi hao wakithibitisha kurusha roketi hiyo.

Makao yaliyolengwa na waasi hawa ni pamoja na mahakama ya kifalme na ofisi ya mfalme wa Saudi Arabia.

Hata hivyo dakika chache baadae kituo cha televisheni ya taifa kiliripoti kuwa roketi hiyo ilidunguliwa kusini mwa mji mkuu Riyadh.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.